Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amemkashifu rais Uhuru Kenyatta akidai serikali yake inadandia miradi isiyokuwa yake kwa nia ya kujipatia umaarufu.
Akizungumza akiwa katika jukwaa moja na rais Kenyatta mjini Mombasa, Joho alidai kuwa miradi ambayo serikali ya jubilee inazindua ilianzishwa na serikali ya awali.
Matamshi yake yalikuja saa chache baada ya rais Kunyatta kuzindua kivukio cha waenda kwa miguu-foot bridge, eneo la Buxton mjini Mombasa.