Washukiwa wa ujambazi wanaswa eneo la Likoni

0
1269

Mombasa,KENYA:Idara ya usalama Mombasa inasema imewakamatwa washukiwa wanne wa ujambazi eneo Likoni.

Wanne hao -wanawake wawili na wanaume 2 wamekamatwa wakiwa chumba kimoja cha kukodi huku mmoja wao akisemekana kuwa na majeraha ya risasi mwilini baada ya kunusurika kifo kutokana na tukio la wizi.

Polisi inasema wawili kati yao wako katika orodha ya washukiwa sugu wanaosakwa na polisi.

Mkuu wa upelelzi likoni Henry Ndombi amesema washukiwa hao walikamatwa na kikosi maalum Cha polisi baada ya kupashwa taarifa na umma.

Comments

comments