Wasichana wa shule wapewa visodo Kilifi

0
1390

Kilifi,KENYA: Wanawake kutoka kundi moja la kijamii kaunti ya Kilifi limeanzisha mradi wa ugavi wa visodo kwa wasichana katika shule za msingi na upili.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kundi hilo la Kilifi Mums-Kibibi Ali, mradi huo unalenga kuwasaidia pia wale wasichana wanaotoka katika familia zisizojiweza.

Amesema wasichana wanaotoka katika familia maskini hulazimika kushiriki mapenzi ili wapate pesa za kununua visodo.

Ameongeza kwamba mradi huo wa ugavi wa visodo unalenga kuwaepusha wahusika kujiingiza katika mapenzi kabla ya wakati na hatimaye kupata mimba mapema.

Comments

comments