Wanakijiji wamsaka “Mchawi wa kutumia nyoka” Rabai

0
1840

Kilifi,KENYA: Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Miereni-Rabai kaunti ya Kilifi baada ya mwanamume mmoja anayeshukiwa kusababisha kifo cha mwanamke kwa njia ya ushirikina kufumaniwa.

Duru za habari zinasema kuwa mwanamume huyo anashukiwa kuhusika na kifo cha mwanamke huyo ambaye aliumwa na nyoka wiki jana na kufariki.

Leo alfajiri inaarifiwa kuwa wanakijiji wamevamia makazi yake kwa lengo la kumshambulia lakini akatoroka.

Aidha bidhaa za ushirikina zikiwemo vichwa vya nyoka vinadaiwa kupatikana ndani ya nyumba yake.

Chifu wa eneo hilo ameripotiwa kufika kwa boma la mshukiwa kujaribu kutuliza hamaki za wanakijiji hao ambao wamesikika wakitishia kumwua mshukiwa popote atakapopatikana.

Comments

comments