Simba asakwa kwa kuwauwa mbuzi sita Magarini

0
1375

Kilifi,KENYA: Shirika la huduma kwa wanyama pori nchini KWS katika maeneo ya Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi linaendeleza msako wa kumnasa simba ambaye alivamia na kuwauwa mbuzi sita katika eneo la Adu huko Magarini.

Afisa mkuu wa KWS tawi la Malindi na Magarini Jane Gitau amethibititha kisa hicho huku akisema kuwa simba mwengine awali alimuua mwanafunzi katika kijiji cha Kulesa huko Adu hali ambayo imewatia hofu wakaazi na wanafunzi wanaorauka kwenda shule eneo hilo.

Aidha afisa huyo wa KWS amesema kuwa uvamizi wa mara kwa mara wa Simba katika maeneo ya makaazi huenda umesababishwa na kukatwa kwa msitu wa Dakacha kwa uchomaji makaa ambao umesababisha jangwa na kupelekea wanyama wengi kutoroka mbugani.

Comments

comments