Polisi waanza msako dhidi ya genge hatari Magarini

0
2250
A police vehicle.A police officer was on Monday arrested after threatening to shoot his love rival PHOTO COURTESY
Polisi eneo la Magarini kaskazini mwa Kaunti ya Kilifi wanasema kuwa wanaendeleza  msako mkali dhidi ya genge la watu wanaotekeleza mauaji ya kiholela katika eneo hilo.
Hadi mwishoni mwa juma lililopita kiasi cha watu watatu walikuwa wameuawa kinyama na watu hao na kisha kutorokea kusikojulikana.
Taarifa za polisi zinasema inahofiwa huenda watu hao wakawa in miongoni mwa genge lililoibuka majuzi linalolenga kuuwa wazee kwa tuhuma za uchawi na kupora mali hasa katika vituo vya mafuta.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama eneo hilo Simon Lokorio ameambia Baraka FM kwa njia ya simu kwamba vyombo vya Sheria vimepania kuwakamata watu hao kivyovyote vile.
Amesema watu waliotekeleza mauaji eneo la Sabaki ndio haohao waliotekeleza mauaji eneo la Gongoni.
Watu waliouawa juma lililopita in mabawabu wawili wa vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na mtu mmoja eneo la Sabaki na Gongoni.
Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijabainika ila polisi inaomba raia kutoa ripoti muhimu kuhusu watu hao.

Comments

comments