Kamishna wa kaunti ya Lamu awaonya wanasiasa

Kamishna wa kaunti ya Lamu awaonya wanasiasa

by -
0 282

Lamu,KENYA:Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Joseph Kanyiri, ametoa onyo kali kwa  wanasiasa  wa Lamu dhidi ya kuchochea wananchi hasa msimu huu wa sherehe.

Kanyiri anasema msimu huu wa sherehe za Mwezi Disemba, wanasiasa wengi wamekuwa wakizuru maeneo tofauti ya Lamu kukutana na wakazi na hata kuwapa zawadi za kufunga mwaka.

Anasema ofisi yake iko macho na kwamba inafuatilia kwa karibu mienendo ya wanasiasa hao.

Amewataka wakazi wa Lamu kujiepusha na viongozi ambao lengo lao ni kuwagawanya kwa misingi ya kikabila au dini.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES