Barabara ya Mombasa ambayo wapita njia hawajali usalama wao

0
2072
Barabara ya Changamwe inayoelekea uwanja wa ndege wa Moi. PICHA: GEORGE OTIENO

Huku miundo mbinu ikiendelea kama vile barabara pana kubadilisha taswira ya eneo la Changamwe hapa Mombasa, wakazi wengi na wasafiri wanaonekana kukiuka sheria za barabara.

Uchunguzi wa Baraka FM umebaini kuwa licha ya barabara hiyo kuwa na daraja la miguu, wakenya wengi bado wanahatarisha maisha yao kwa kuvuka barabara pasipofaa.

Aidha wenye magari na mikokoteni pia wanakiuka sheria za trafiki kwa kutumia pande zisizofaa barabarani bila kujali.

Wenye pikipiki pia hawajawachwa nyuma katika uvunjaji wa sheria hasa kwenye barabara hio mpya.

Wakati mwandishi huyu akifanya uchunguzi, wapita njia na hata wanaosukuma mikokoteni walionekana wakivuka barabara pasi na kujali.

Mama mmoja baada ya kuvuka barabara pasipo faa, akaanza kujifuta miguu barabarani bila kujali magari yaliyokuwa yakipita kwa kasi.

Kando kidogo, watoto ambao huenda ni wa sehemu hiyo, wanasusia kuvuka barabara kupitia daraja hilo na badala yake wanatizama magari kabla ya kutimka mbio hadi sehemu ya pili.

Mkaazi mmoja ambaye hakutaka kutajwa alisema daraja hilo linawapotezea wakati.Wanasema kuvuka barabara popote ni njia ya mkato.

” Bridge iko mbali sana.Kuenda mpaka huko ndipo nivuke ntapoteza muda mwingi.heri nikate tu na hapa”, alinukuliwa akisema.

Comments

comments