Wachonga vinyago Malindi walilia soko

0
1055

Wachongaji wa vinyago mjini Malindi kaunti ya Kilifi wanalalamikia kuzorota kwa sekta hiyo tangu mlipuko wa virusi vya corona nchini.

Wafanyabisahara hao wanasema wamekosa soko la bidhaa zao kwani sekta ya utalii imeathirika pakubwa kutokana na janga hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Muyeye, wachongaji hao wakiongozwa na mwenyekiti Cosmas Kyalo, wameiomba serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuwatafutia soko la bidhaa zao.

Comments

comments