Mpishi wa shule ya upili ya Kambe ajitia kitanzi

0
1573

Mpishi wa shule ya upili ya Kambe huko Rabai amefariki kwa kile kinachosemekana amejitia kitanzi.

 Mwili wa mpishi huyo mwanamume mwenye miaka 40 umepatikana mapema leo shuleni humo.

Kufikia sasa haijabainika chanzo cha marehemu kujiua.

Chifu wa lokesheni ya Kambe Harrison Mtsonga, amesema huenda mpishi huyo alikuwa na matatizo ya kinyumbani yaliyompelekea kujiua.

“Hakukuwa na shida kati yake na shule.Pengine ni masuala ya kinyumbani, alisema chifu.

Marehemu amewaacha watoto wanne akiwemo mmoja ambaye ni mwanafunzi katika shule hiyo.

Polisi walifika na kuondoa mwili wa marehemu.

Comments

comments