Mwanamume ashtakiwa kwa kumnajisi binti wa miaka 13

0
1474

Mombasa,KENYA: Mwanaume mmoja amefikishwa kortini  Mombasa  akishtakiwa kwa kosa la kumnajisi msichana wa miaka 13.

Felix Otieno Mito anadaiwa kutekeleza unyama huo  katika  mtaa wa Owino Uhuru eneo bunge Jomvu.

Lakini amekana mashtaka mbele ya  hakimu mkuu Julius Nang’ea.

Ameachiliwa kwa dhamana ya shillingi laki tatu, huku kesi ikisubiri kutajwa tarehe 11 mwezi huu.

Comments

comments