Polisi wa Watamu wadaiwa kumpiga na kumjeruhi mkaazi

0
1771

Mwanamume kutoka eneo la Watamu huko Malindi kaunti ya Kilifi anaomba haki itendeke baada ya kudaiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya na polisi.

Mwanamme huyo kwa jina Ali Shedrack anadai alivamiwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Watamu waliokuwa wakishika doria na kumpiga na kujeruhi vibaya jicho lake.

Anadai polisi katika kituo hicho cha Watamu walidinda kuandikisha taarifa ya malalamishi.

Kwa upande wake OCS wa kituo hicho cha polisi cha Watamu Raphael Mwela amewaondolea lawama maafisa wake na kusema hawakuhusika hivyo kumtaka mlalamishi kutafuta usaidizi katika kituo cha polisi cha Malindi, akisema oparesheni ilifanywa na maafisa wa kituo cha polisi wa Malindi.

Comments

comments