Onyo kwa watoto wanaorandaranda baharini

0
1174

Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo ameonya kuwa watoto watakaopatikana wakizurura katika fuo za bahari baada ya saa kumi na mbili jioni watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akiwahutubia waandishi wa habari, Ngumo amewahimiza wazazi kuwajibikia majukumu yao ipasavyo kwa kuwalinda watoto wao ili kuwaokoa kutokana na maovu katika msimu huu wa likizo.

Aidha amesema kuwa wazazi watakaokosa kuwajibikia mienendo ya watoto wao watashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Comments

comments