Watu wanaohusika katika udanganyifu wa mitihani ya kitaifa wanafaa kunyongwa.
Hayo ni kwa mujibu wa mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili-Wallah Bin Wallah.
Katika mahojiano ya kipekee na Baraka FM hapa Mombasa, Wallah Bin Wallah anadai kuwa sifa ya Kenya imeharibika kutokana na wizi wa mitihani.
Anasema adhabu hiyo kali itakomesha tabia hiyo na hivyo kusafisha hadhi ya Kenya katika ulingo wa kimataifa.
Waziri wa elimu Amina Mohammed alionya kuwa walimu , wazazi pamoja na wanafunzi watakaopatikana kuiba mitihani watabeba msalaba wao wenyewe.