Wazazi:Hatutaki mgomo wa walimu msimu wa mtihani

0
993

Mombasa, KENYA: Katibu mkuu wa muungano wa chama cha kutetea walimu knut nchini sosion ametakiwa kuwapa wanafunzi muda kukamilisha mitihani yao ya kitaifa kabla kuanza harakati zao za mgomo.

Mwanaharakati wa elimu hapa Mombasa- Ben Oluoch amesema mgomo ukiitishwa wakati huu, huenda ukaathiri watahiniwa.

Kulingana na  Oluoch itakua jambo la kusikitisha kwa wazazi kulipa karo na mwishowe watoto wao kutatizwa na mgomo.

Hata  hivyo Oluoch amemtaka waziri wa elimu Bi.Amina Mohammed kuingilia kati na kutatua tofauti iliyoko baina yao ili watoto wasiweze kuathirika.

Comments

comments