Gavana Obado kuzuiliwa rumande kuhusu mauaji

0
843

Nairobi,KENYA:Gavana wa Migori Okoth Obado ataendelea kuzuiliwa rumande.

Mahakama imesema itatoa umauzi jumanne(kesho) iwapo Obado ataachiliwa kwa dhamana au la.

Aidha Obado amekana mashtaka ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno.

Bi.Sharon alipatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika msitu wa Kodera kaunti ya Homabay mapema mwezi huu wa Septemba.

Uchunguzi wa chembechembe za DNA ulibaini kuwa gavana huyo ndiye alimyemtunga mimba msichana huyo.

Comments

comments