Wakenya kujua hatma yao bunge likijadili ushuru wa mafuta

0
1147

Bunge la kitaifa leo linatarajiwa kupiga kura kuidhinisha au kukataa mswada wa fedha ambao unapendekeza ushuru wa asilimia 8 kwa bidhaa za mafuta.

Rais Kenyatta alipendekeza ushuru wa asilimia 8 badala ya 16.

Iwapo mswada huo utapata uungwaji mkono, ushuru wa mafuta utapanda.

Muungano wa Nasa ulitangaza kuwa utaunga mkono mswada huo sawia na jubilee.

Lakini baadhi ya wabunge walidokeza kuwa hawatotishwa kuunga mkono mswada huo wakisema ni mzigo kwa wakenya.

Hayo yakijiri wakenya bado wanalalamikia bei ya juu ya bidhaa .

Hapa Mombasa, baadhi ya wakaazi wanasema kuwa ushuru huo wa asilimia 8 bado ni mzigo kwa wananchi wa kawaida.

Wafanyabiashara nao pia wanalamika wakidai kuwa biashara zao zimedorora ikilinganishwa na hapo awali

Comments

comments