Wavuvi wanne wa Kisauni wapotea baharini

0
1322

MOMBASA: Wavuvi wanne eneo la Nyali hawajulikana walipo baada ya mashua yao kupinduka siku ya jumanne.

Kamanda wa polisi Mombasa Johnstone Ipara amesema kuwa mashua ya wavuvi hao ilipinduka Jumanne saa tano usiku wakiwa kilomita 10 ndani ya bahari.

Aidha Ipara amesema kuwa wavuvi wawili walifaulu kuogelea huku wanne wakisombwa na maji.

Mashua hiyo ilipinduka kufuatia mawimbi makali yalioshuhudiwa baharini.

Polisi wamesema tayari wanaendelea na oparesheni kutafuta miili ya wanne hao.

Wavuvi hao walikuwa wametoka eneo la Kisauni.

Comments

comments