Muuza nyama ya paka apunguziwe kifungo jela

0
1320

Mtu aliyeuzia watu nyama ya paka eneo la Nakuru amepunguziwa hukumu ya jela.

Awali mtu huyo kwa jina James Kimani alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela lakini sasa mahakama imepunguza hadi miaka miwili.

Jaji Joel Ngugi amesema mshatkiwa huyo anatumikia vifungo vyake kwa wakati mmoja.

Jaji Ngugi pia amesema mahakama ya chini ilifanya makosa kwa kumpiga mtu huyo  faini ya shilingi elfu 50 badala ya shilingi elfu 10.

Comments

comments