Polisi wawapiga risasi wahalifu wa wakali kwanza Kisauni

0
1560

Mombasa,KENYA: Polisi wanasema wamewauwa kwa kuwapiga risasi washukiwa wawili wa kundi la kihalifu eneo la Magodorni Kisauni hapa Mombasa.

Hii inakuja saa chache baada ya afisa wa CID aliyedungwa kisu na wahalifu hao kufariki akitibiwa hospitalini.

Washukiwa hao wawili wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la kihalifu la wakali kwanza.

Polisi wanasema walikuwa wamejihami kwa panga na ni miongoni mwa kundi lililomdunga kisu afisa huyo wa CID.

Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Sangura Musee amesema wanawasaka wengine.

Comments

comments