Mkurugenzi wa NYS Richard Ndubai akamatwa kuhusu ufisadi wa sh 9b

0
1173

Mkurugenzi wa NYS Richard Ndubai ametiwa nguvuni na polisi kuhusu sakata ya shilingi bilioni 9 katika shirika hilo.

Kamata kamata imeanza  baada ya  Mkuu wa idara ya upelezi CID -George Kinoti kukabidhi faili 10 zenye majina ya washukiwa wa sakata hiyo ya NYS kwa idara ya mashtaka ya umma.

Ndubai  alikamatwa jumapili usiku na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na naibu mkurugenzi Sam Michuki, mkuu wa idara ya fedha na afisa mwingine ambaye hajatambuliwa.

Tayari watu 40 wameandikisha taarifa kuhusiana na sakata ya ufisadi katika shirika hilo.

Mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji amesema kwa sasa wanachunguza faili hizo moja baada ya nyingine.

Comments

comments