Simba waleta kero eneo la Ganze

0
852

Kilifi,KENYA: Simba wawili wamevamia kijiji cha Mitzedzini kaunti ndogo ya Ganze na kuua ngombe wawili na kumjeruhi mmoja siku moja tu baada ya simba mmoja kuua mbuzi katika kijiji cha Gumara katika eneo hilo.

Chifu wa eneo hilo Samson Thabu amesema kuwa simba hao walivamia zizi la ngombe na kuwaua ngombe hao na wakatoroka baada ya wananchi kuanza kuwakabili.

Maafisa wa idara ya wanyamapori walifika katika eneo hilo na kwa sasa wameanza kuwasaka simba hao ambao kwa sasa wamekuwa tishio kwa usalama wa wananchi.

Wananchi kwa sasa wanaendelea kuishi kwa hofu ya kuvamiwa huku tayari wakiwa wamesitisha shughuli zao za usiku na asubuhi.

Comments

comments