Mamake mtangazaji wa Baraka FM Mnyazi Kakinda azikwa Chonyi

0
1979

Kilifi,KENYA: Watangazaji wa Baraka fm jumamosi walikuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji wa mamake mfanyakazi mwenzao Roselyn Mnyazi Kakinda.

Maziko hayo ya Beatrice Chao Kakinda, yalifanyika siku ya jumamosi katika kijiji cha Silala-Chonyi kaunti ya Kilifi.

Bi. Chao Kakinda aliugua kwa muda kabla ya kuaga dunia yapata wiki mbili zilizopita.

Mamia ya mashabiki wa Baraka fm pia walihudhuria mazishi hayo ya mamake mtangazaji huyo wa kipindi maarufu cha bango mdobwedo reloaded.

Waandishi wa habari kutoka vituo vingine pia walihudhuria maziko hayo yaliyoongozwa na kanisa katoliki.

Baraka FM inawatakia familia ya Kakinda faraja wakati huu mgumu.

Comments

comments