Kalonzo aishtaki serikali ya jubilee kuhusu bunduki

0
1113

Nairobi,KENYA: Kinara wa Wiper – Kalonzo Musyoka  sasa ameishtaki serikali kwa kumnyang’anya walinzi na leseni ya bunduki.

Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya Milimani, Kalonzo anataka serikali izuiwe kumpokonya leseni ya bunduki na pia kumregeshea walinzi wake.

Kalonzo ni mmoja wa vinara wa Nasa ambao wamelengwa na serikali kuhusu mchakato wa uapisho wa Raila Odinga.

Kalonzo anasema anastahili ulinzi kwani alikuwa makamu wa rais kati ya mwaka 2008-2013.

Comments

comments