Kura zaanza kuhesabiwa upya Changamwe na Lamu

0
1088

Mombasa,KENYA: Zoezi la kuhesabu upya kura za kiti cha ubunge wa  Changamwe limeanza rasmi kufuatia agizo la mahakama kuu ya Mombasa.

Hii ni bada ya jaji Njoki Mwangi kuagiza kura za vituo 58 kuhesabiwa upya kufuatia madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti nane mwaka jaa.

Jaji Mwangi aliagiza hakimu Janet Kassam kusimamia zoezi hilo chini ya siku tano na kutoa ripoti kortini tarehe 24 mwezi huu.

Hata hivyo waandishi wa habari walizuiliwa kushuhudia zoezi hilo ambalo litafanyika kwa muda wa siku 5 eneo la Shimanzi  hapa Mombasa.

Kwingineko awamu ya pili ya marudio ya kuhesabiwa kura za ubunge wa Lamu Magharibi imeendelea katika kituo kikuu cha kuhesabu kura mjini Mokowe baada ya zoezi hilo kung’oa nanga rasmi jumatano.

Shughuli hiyo inatekelezwa kufuatia amri ya mahakama kwamba masanduku zaidi yanayohifadhi kura za uchaguzi mkuu wa Agosti 8 yafunguliwe na kura kuhesabiwa upya.

Awamu ya kwanza ya kuhesabiwa upya kwa kura hizo ilikamilika majuma mawili yaliyopita, ambapo jumla ya masanduku 43 pekee kati ya 123 yalifunguliwa na kura kuhesabiwa.

 RISHAD AMANA APINGA USHINDI WA MUTHAMA

Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilimtangaza, Stanley Muthama wa chama cha Maendeleo Chap Chap kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kujizolea jumla ya kura 11,090 ilhali, Rishad Amana wa chama cha ODM akiibuka wa pili kwa kura 10,950.

Amana aidha alipinga matokeo hayo kortini kwa madai kwamba kura zake ziliibwa waziwazi vituoni, malalamishi ambayo yalipelekea korti kuelekeza kura hizo kuhesabiwa upya.

Comments

comments