Taita Taveta, KENYA: Gasper Kabaka ambaye aliteuliwa na gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granron Samboja kuchukua nafasi ya waziri maji amehojiwa na bunge la kaunti hiyo.
Kabaka aliileza kamati ya bunge kwamba atahakikisha kampuni ya usambazaji wa maji katika kaunti hiyo [TAVEVO] inawajibika.
Ameahidi kukabiliana na changamoto zote za maji ili kufaidisha wamananchi iwapo atachaguliwa katika wadhifa huo.
Bunge hilo pia limempiga msasa aliyeteuliwa kwa nafasi ya nyumba barabara na miundo msingi Houghton Msagha.
Wawili hao waliteuliwa upya na gavana samboja baada ya wengine kutopitishwa na bunge hilo.