Marekani yampongeza rais Kenyatta

0
2451

Nairobi,KENYA:Serikali ya Marekani imempongeza rais Uhuru Kenyatta kwa kuapishwa rais kwa muhula wa pili na wa mwisho.

Kupitia barua, serikali hiyo ya Marekani Pia imesema iko tayari kushirikiana na Kenya katika kuleta uponyaji baada ya joto la kisiasa lililoshuhudiwa wakati wa uchaguzi.

Aidha pia imeeleza kusikitishwa na hatua ya vyombo vya usalama kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.

Rais Kenyatta aliapishwa jana ambapo ameahidi kuhudumia wananchi kwa usawa na pia kuhimiza amani na utangamano.

Comments

comments