Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa leo

0
2807

Nairobi,KENYA:Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kuhudumu muhula wake wa pili na wa mwisho.

Hafla hiyo imeongozwa na jaji mkuu David Maraga katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Naibu rais William Ruto pia ameapishwa.

Marais kadhaa kutoka bara Afrika pia wamehudhuria hafla hiyo wakiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda,Salva Kiir wa Sudan kusini.

Wengine ni Ian Khama wa Botswana, Omar Guelleh wa Djibouti na Ali Bongo Ondima wa Gabon.

Awali Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya polisi kurusha vitoa machozi nje ya lango kuu la uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambako rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa.

Polisi waliwarushia vitoa machozi baada ya halaiki ya watu kung’ang’ana kuingia kwa lazima ndani ya uwanja huo licha ya kuwa tayari umejaa.

Maafisa wa uokoaji walionekana wakiwabeba majeruhi kadhaa kwenye machela.

Na huko Jacaranda, polisi walitibua jaribio la wafuasi wa NASA kuandaa mkutano sambamba na uapisho wa rais.

Polisi walitumia vitoa machozi na kuwatimua wafuasi hao.

Aidha inadaiwa kuwa watu wasiojulikana walimwaga kinyesi uwanjani humo usiku kuzuia mkutano huo.

Kinara wa NASA Raila Odinga alisema watapuuza onyo la polisi kukongamana uwanjani huo.

Comments

comments