Serikali kuwatuza wakuu wa shule zilizofana katika KCPE

0
840

Mombasa,KENYA: Ikiwa wewe ni mwalimu mkuu wa shule iliyofana katika mtihani wa KCPE subiri zawadi yako.

Waziri wa kitaifa wa elimu Fred Matiang’i anasema serikali itawatunuku walimu wakuu wa shule za msingi za umma ambazo zilifanya vizuri katika mtihani wa kitaifa KCPE.

Waziri Matiang’i amesema serikali imeanzisha mpango huo kama njia moja ya kuwapa walimu motisha kutokana na utendakazi bora.

Ameongeza kuwa shule hizo pia zitapata msaada kutoka kwa serikali ili kuboresha miundo mbinu kama vile viwanja vya michezo na madarasa.

Waziri huyo amedokeza kuwa watashirikiana na tume ya huduma kwa walimu (TSC) kumtunuku kivyake mwalimu mkuu aliyeibuka bora.

Comments

comments