Askofu wa kanisa la katoliki jimbo la Eldoret Cornel Korir amezikwa jumamosi,mazishi yaliohudhuriwa na rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto,magavana pamoja na viongozi wengine.
Katika rambirambi zake rais Uhuru Kenyatta aliwahakikishia wakenya kuwa atatumia mbinu zote kuhakikisha kuwa amani imedumishwa nchini.
Rais Kenyatta amewataka viongozi wa kanisa kushirikiana na serikali kuhakikisha amani imerejeshwa nchini.
Naye naibu rais William Ruto alimtaja askofu Korir kama shujaa wa amani katika taifa la Kenya.
Aidha alisisitiza kuwa kama viongozi wataendelea kuhimiza amani kama njia ya kumkumbuka askofu huyo.
Marehemu aliaga dunia mwezi jana katika hospitali ya rufaa ya Moi Eldoret baada ya kuugua kwa muda mfupi na atakumbukwa kwa juhudi zake za kuhimiza amani.