Marwa awaonya wanajeshi wanaopigana na Al-shabaab Lamu

0
1536

Lamu,KENYA: Mshirikishi wa ukanda wa pwani Nelso Marwa ameonya jeshi KDF dhidi ya kuzembea katika kumliza magaidi wa Al-shaaba katika msitu wa boni kaunti ya Lamu.

Marwa amesema anashangaa ni kwanini oparesheni ya linda boni  imechukua muda wa miaka miwili lakini hakuna mafanikio.

Amelaani vikali mauaji ya watu wanne siku ya ijumaa ambapo kundi la Al-shabaab linalaumiwa.

Pia ameagiza uchunguzi dhidi ya maafisa wa usalama wa Hindi na Mokowe kufuatia mauaji hayo akisema huenda walizembea majukumu yao.

Comments

comments