Mbunge Babu Owino azua kioja bungeni!

0
2087

Nairobi,KENYA:Mbunge wa Embakasi mashariki Paul Ongili maarufu kama Babu Owino alizua kioja bungeni wakati wa kuapishwa.

Owino aliazimika kurudia kiapo cha kuapishwa bungeni.

Hii ni baada ya kutaja jina la kinara wa NASA Raila Odinga kwenye kiapo kinyume na sheria.

Aidha wakati wa kutamatisha kula kiapo, kwa mara nyingine mbunge huyo alitamka neno “Tibim”, ambalo limekua kama kibwagizo cha upinzani wakati wa kampeni.

Wakati huo huo aliyekuwa gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka amechaguliwa kwa wingi wa kura kuwa spika wa bunge la seneti.

Lusaka alipata kura 42 akifuatwa na Farah Maalim aliyepata kura 25.

Alishinda katika duru ya pili ya uchaguzi huo baada ya kukosekana mshindi katika duru ya kwanza.

Duru ya kwanza Lusaka alipata kura 40 dhidi ya Maalim aliyekuwa na kura 26.

 

Comments

comments