Nairobi,KENYA:Waziri wa ugatuzi Mwangi Kiunjuri ametangaza tarehe ambapo magavana wataanza kuapishwa.
Amesema kuwa gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ataapishwa tarehe 22 mwezi huu wa 8 katika uwanja wa Mama Ngina.
Naye gavana wa Kilifi Amerson Kingi na mwenzake wa Kwale Salim mvurya wataapishwa tarehe 21 mjini Kilifi na Kwale mtawalia.
Magavana wa Taita Taveta Granton Samboja na mwenzake wa Tana River Dhadho Gohdana pamoja na Fahim Twaha wa Lamu pia wataapishwa tarehe 21 mwezi huu wa nane.
Aidha waziri Kiunjuri amedokeza kuwa magavana wanaoondoka ofisini watalipwa marupurupu ya muda waliohudumu kwa mujibu wa sheria.