Mshukiwa wa ujambazi achomwa moto na wananchi

0
1304
Polisi wakishika doria Likoni.

Likoni,MOMBASA: Mshukiwa wa ujambazi ameuawa na umati wa watu huko Likoni karibu na shule ya upili ya likoni.

Mshukiwa ambaye ametambuliwa kwa jina la utani Tinted alipigwa na kisha kuchomwa na umati huo wa watu waliokuwa na ghadhabu.

Mkuu wa polisi likoni Benjamin Rotich alisema mshukiwa alikuwa katika orodha ya majambazi sugu wanaosakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na uhalifu.

Rotich alisema mshukiwa huyo amekuwa akiongoza genge la washukiwa watatu hatari na kwamba wanawasaka wenzake wengine wawili.

Washukiwa wawili wanaoaminika kuwa wafuasi wa genge la wakali kwanza walikamatwa eneo la Kongowea kisauni kwa madai ya kutaka kuchoma soko kuu la Kongowea.

Mkuu wa polisi kisauni Christopher Rotich aliambia Baraka Fm kuwa washukiwa hao walikuwa na silaha na petroli na wamekamatwa na polisi waliokuwa wakishika doria katika soko hilo tangu matokeo ya urais yatangazwe Ijumaa.

Rotich alisema usalama umeimarishwa zaidi eneo hilo huku polisi wa ziada wakiongezwa.
Amesema washukiwa watashtakiwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.

Comments

comments