Kampeni kuangamiza mji wa kale wa Lamu

0
1983
A street in UNESCO listed Lamu old town. PHOTO/ FILE.

Lamu,KENYA:Ukale katika mji wa kihistoria wa Lamu unazidi kuhatarishwa hasa msimu huu ambapo kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti 8 zinazidi kupamba.

Kulingana na sheria zilizoko, wakazi wa kisiwa cha Lamu hawaruhusiwi kutumia magari, pikipiki wala baiskeli katika kutekeleza shughuli zao za kila siku mjini humo.

Wakazi wanaoruhusiwa mjini humo ni wale ambao hutembea kwa miguu au kwa kutumia punda pekee.

Mnamo 2001, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO liliorodhesha mji wa kale wa Lamu kuwa miongoni mwa sehemu zinazotambulika kote ulimwenguni kwa kuhifadhi.

Hata hivyo tangu kampeni za uchaguzi wa Agosti 8 kuanza, kumeshuhudiwa uvunjaji wa sheria zinazopiga marufuku matumizi ya magari, pikipiki na baiskeli mjini humo huku wakazi wakizidi kutumia vyombo hivyo kwa wingi bila kutatizwa.

Kwa sasa zaidi ya magari 30, pikipiki zaidi ya 50 na baiskeli zaidi ya 100 zinahudumu kwenye mji huo wa kale, hivyo kupelekea msongamano wa watu na vifaa hivyo mjini humo.

Wanasiasa wanaofanya kampeni pia wametumia mwanya huo kuleta magari ya kutekelezea kampeni zao ndani ya mji wa Lamu, jambo ambalo linazidi kubadili sura ya mji huo wa kale.

Comments

comments