Mwanamme amnyofua mvulana sehemu za siri huko Wundanyi

0
2090

Taita Taveta,KENYA:Mvulana wa umri wa miaka mitano amelazwa na majeraha katika hosipitali ya Nairobi Women  baada ya mjomba wake kumkata sehemu za siri kule Wundanyi katika kaunti ya Taita-Taveta.

Kitendo hicho kilitokea Jumanne usiku katika mtaa wa  Matasenyi baada ya kuripotiwa kuwa manusura alikuwa ameambatana na mjomba wake.

Mkuu wa polisi Wundanyi  OCPD Benjamin  Muhia amesema kuwa mshukiwa alimjeruhi kijana punde tu alipotoka shule alichukua kisu na kung’ofua sehemu nyeti bila sababu muhimu.

OCPD anasema kwamba mshukiwa alipigwa na umati uliokuwa na hamaki na kupelekwa kwenye kituo cha polisi akiwa hali maututi ambapo alipelekwa katika hosipitali ya polisi ya Dawida  na kisha akahamishiwa hosipitali ya kaunti ndogo ya Wesu huku uchunguzi ukiendelea.

Comments

comments