Mtoto afariki kisimani huku mwengine akinyofolewa sehemu nyeti

0
2192

Lamu,KENYA:Mwili wa mtoto wa umri wa miaka 7 aliyeanguka ndani ya kisima umepatikana eneo la Kithanguni Kikuyu huko Mkomani kaunti ya Lamu.

Kulingana na babake, mwanae alitoweka jana jioni na juhudi za kumtafuta zilikua zikiendelea.

Mwili wake umepatikana leo wakati babake akielekea kuteka maji leo asubuhi.

Lakini wakazi wanadai kuwa huenda mtoto huyo aliuawa kwingineko kasha mwili wake kutupwa ndani ya kisima hicho.

Mwili wake umepelekwa katika hospitali ya King Fahad kwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo.

Kwingineko mtoto wa  umri wa miaka mitano anauguza majeraha baada ya kunyofolewa nyeti zake na mjombaje, eneo la kese wadi ya werugha iliyoko mjini wundanyi.

Haijabainika mara moja kilichomshinikiza mhusika kutekeleza kitendo hiki cha unyama ambacho  kimelaaniwa pakubwa na wananchi.

kwa sasa polisi wameanza kumsaka mshukiwa ambaye alitoweka punde tu baada kutekeleza unyama huo.

Mtoto huyo amesafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu ya dharura.

 

Taarifa zaidi na Fatuma Rashid kutoka Taita Taveta

 

Comments

comments