Seneta Muthama ajiuzulu kutoka chama cha Wiper

0
1457

Nairobi,KENYA: Seneta wa Machakos Johnson Muthama amejiuzulu kutoka chama cha Wiper kwa kile anachodai ni usimamizi mbaya wa chama.

Muthama alisema hatowania wadhifa wa useneta kaunti ya Machakos kwa muhula wa pili  lakini ataendelea kupigia debe mgombea wa urais kupitia mrengo nwa NASA Raila Odinga.

Aidha amekashifu viongozi wa Wiper kwa kuwapendelea wagombea katika uchaguzi wa mchujo uliokamilika majuzi.

Muthama aliwakilisha chama cha Wiper katika kamati iliyokuwa imepewa jukumu la kumtambua  atakayepeperusha bendera ya urais katika mrengo wa NASA.

Comments

comments