Mtaala mpya wa elimu wa 2-6-3-3-3 kufanyiwa majaribio

0
3575

Mombasa,KENYA:Wizara ya elimu inaanza kufanyia majaribio  mtaala mpya wa elimu wa 2-6-3-3-3 nchini.

Waziri wa elimu Fred Matiang’I alisema kuwa mtaala huo mpya utafanyiwa majaribio katika shule 400 nchini kuanzia mwezi huu wa mei.

Wadau wamekuwa wakishinikiza mtaala wa 8-4-4 ubadilishwe wakisema hauzingatii ujuzi wa mwanafunzi ila kupita masomo.

Chini ya mfumo huu wa 2-6-3-3-3, mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE yataondolewa na badala yake wanafunzi watakuwa wakifanya mitihani ya mwisho wa muhula.

Wakati huo huo Afisa wa mipangilio katika shirika la kijamii linaloshughulikia elimu ya mtoto wa kike la KWEA kaunti ya Kwale Salim Mwatenga anasema kuwa mtaala huo unalenga  kuinua viwango vya elimu  na kuboresha maisha ya baadae ya wanafunzi  kinyume  na ilivyo sasa.

Comments

comments