MCA wa ODM aliyeaga dunia kuzikwa Mtwapa-Kilifi

0
2614
The late Bakari Ali in his campaign poster PHOTO COURTESY

Mombasa,KENYA:Mwakilishi wa wadi ya Shimo la Tewa hapa Mombasa-Bakari Ali Munyi aliyeaga dunia jana (jumatatu) atazikwa leo(jumanne).

Maziko yake yatafanyika eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi kwa kuzingatia dini ya kiislamu.

Munyi alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa ndani ya basi akiwa safarini kuelekea Nairobi kuwasilisha makaratasi yake ya uteuzi.

MCA huyo alishindwa katika kura ya mchujo ya chama cha ODM majuzi.

Marehemu alipanga kutetea kiti chake kama mgombea huru katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.

Comments

comments