Kalonzo Musyoka ashurutisha ODM kumwomba msamaha

0
1469

Nairobi,KENYA:Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, sasa anamtaka katibu mkuu wa ODM Agnes Zani aombe msamaha kwa kudai kuwa tayari muungano wa NASA umemchagua mgombea wao wa urais.

Zani anadaiwa kunukuliwa akisema kuwa Raila atakuwa mgombea urais, Kalonzo atakua mgoemba mwenza, Musalia Mudavadi atakuwa waziri mtendaji naye seneta wa Bungoma Moses Wetangula, awe spika wa bunge.

Lakini Kalonzo amekanusha madai hayo akisema hiyo ni njama ya baadhi ya watu wenye nia ya kuleta mvurugano ndani ya NASA.

Kauli yake imeungwa mkono na Mudavadi ambaye anasema kuwa aliyetoa majina ya timu hiyo alikua kitoa maoni yake binafsi na wala sio maafikiano ya NASA.

Muungano huo wa NASA bado haujamtangaza mgombea wake wa urais miezi mine kabla ya uchaguzi mkuu wa agosti.

Comments

comments