Chama cha wiper kupeana tiketi ya moja kwa moja

0
1232

Nairobi,KENYA: Kiongozi wa wachache bungeni Francis Nyenze, amesema chama cha Wiper pia kitawapa wagombea wake tiketi ya moja kwa moja kama ODM ilivyofanya.

Akishtumu ODM kupeana tiketi ya moja kwa moja, Nyenze anasema kuwa hatua hiyo inaumiza demokrasia.

Nyenze ambaye ni mbunge wa Wiper, anasema kuwa ODM kupeana tiketi ya moja kwa moja inaamanisha hakutakuwa na kura ya mchujo ya pamoja kati ya ODM na Wiper.

Ameongeza kwamba iwapo ni Wiper ingekuwa ya kwanza kutoa tiketi ya moja kwa moja, basi ingeshtumiwa vilivyo lakini kwasababu ODM wameshaamua kupeana tiketi zao, basi Wiper nao hawana budi kuendeleza hulka hiyo.

Siku ya jumatatu ODM iliwapa wagombeaji wake 427 tiketi ya moja kwa moja huku kinara Raila Odinga akisema hatua hiyo itawapa fursa mwafaka viongozi hao kupiga kampeni.

Comments

comments