Joho asema cheti chake cha KCSE ni halali

0
1392

Mombasa,KENYA:Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amekanusha madai kuwa cheti chake cha kidato cha 4 KCSE ni ghushi.

Joho anasema hio ni mojawapo ya njama za serikali ya jubilee kumhujumu na kumpiga vita.

Kupitia msemaji wake,Richard Chacha, gavana huyo anasema hamna idara yoyote nchini inayopinga uhalali wa vyeti vyake isipokuwa jubilee.

Msemaji huyo sasa anawataka wenye shauku kuhusu masomo ya gavana Joho, kudhibitisha kupitia shule aliyosomea ya Serani.

Mwanasiasa wa Mombasa-Ananiah Mwaboza alidai kuwa Joho alighushi cheti hicho huku akitaka ashtakiwe.

Comments

comments