Muungano wa NASA wakumbwa na wasiwasi

0
1625

Nairobi,KENYA:Hali ya sitofahamu imegubika muungano wa NASA baada ya mkutano wa vinara wake uliofaa kufanyika kutatua mgogoro kukosa kufanyika.

Duru zinasema kuwa mkutano haukufanyika kwasababu vinara wawili Kalonzo Musyoka na Moses Wetang’ula hawakuwepo.

Inasemekana Kalonzo Musyoka aliondoka nchini kuelekea Dubai akiahidi kurudi mapema kwa mkutano huo lakini hilo halikutimia.

Lakini inasemekana Kalonzo aliondoka nchini baadae ishara kuwa hawezi kurudi kwa wakati ufaao ili kuhudhuria mkutano huo.

Naye  Wetang’ula  anadaiwa kuwafahamisha vinara wenza Raila Odinga na Musalia Mudavadi kuwa hatokuwepo kwani atakua anahudhuria kongamano la bunge hapa Mombasa.

Raila alikatiza ziara yake ya Marekani ili kuandaa vikao vya kukwamua mvutano ambao unasemekana kughubika muungano huo wa NASA.

Comments

comments