Vinara wasema muungano wa NASA uko imara na hautasambaratika

0
1393

Nairobi,KENYA:Viongozi wa muungano wa kisiasa wa NASA wamekanusha taarifa kuwa baadhi yao wanapanga kuusambaratisha muungano huo kwa kuondoka.

Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetang’ula jana jumapili wameeleza wakenya kuwa muugnao huo utabaki imara.

Wakiongea katika mkutano wa kisiasa katika eneo la Kitengelea mjini Nairobi, wanasema lengo lao ni kumwondoa rais Uhuru Kenyatta uongozini katika uchaguzi wa mwezi agosti.

Mudavadi alisema NASA iko imara na kwamba yuko tayari kumwunga mkono atakayechaguliwa kupeperusha bendera ya muungano huo katika kura ya urais.

Wakati huo huo kinara wa ODM Raila Odinga amekatiza ziara yake ya Marekani kurudi nchini kuongoza mazungumzo ya upatanishi ndani ya NASA.

Comments

comments