Je rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alizaliwa wapi?

0
3785

Nairobi,KENYA: Nduguye wa kambo wa rais wa zamani wa Marekani -Malik Obama amezua mjadala kuhusu alikozaliwa Barack Obama huku akitoa kile anachosema ni ushahidi kuwa rais huyo wa zamani alizaliwa humu nchini.

Kulingana na cheti cha kuzaliwa ambacho Malik ameweka kwenye mtandao wake wa twitter, Obama alizaliwa katika hospitali ya mkoa wa Mombasa CPGH maarufu kama Makadara mwaka 1961.

Obama amekua akikana kuwa alizaliwa humu  nchini hatua ambayo ingemzuia kugombea urais wa Marekani mwaka 2008.

Malik Obama  anasema japo anampenda nduguye, anadai kuwa Obama ni mwongo na kwamba amekataa kujitambulisha kama mwafrika mbali na kuwatenga watu wa jamii yake.

Malik Obama ni mfuasi wa rais wa Marekani Donald Trump ambaye aliwahi kuzua mjadala akisema Obama sio mzaliwa wa Marekani hivyo hakupaswa kugombea urais.

OBAMA

Comments

comments