Joho asema hamwogopi Omar Sarai katika mchujo wa pamoja

0
1489

Mombasa,KENYA:Gavana wa Mombasa- Ali Hassan Joho amesema yuko tayari kwa uchaguzi wa mchujo iwapo muungano wa NASA utaamua kufanya mchujo huo.

Akiongea siku ya jumapili baada ya kulakiwa kutoka Marekani, Joho alisema haogopi uchaguzi wa mchujo utakaoshirikisha vyama tanzu vya NASA.

Joho alisema anashindwa ni kwanini wapinzani wake wanaogopa kura ya mchujo wa pamoja.

Matamshi yake yanaonekana kumlenga mpinzani wake mkuu senata wa Mombasa Hassan Omar ambaye alitangaza kuwa chama cha wiper kitafanya mchujo wake kivyake na wala hakitafanya mchujo wa pamoja.

Omar na mbunge wa Nyali -Hezron Awiti wametangaza kuwa watagombea kiti hicho cha ugavana.

Gavana Joho alilakiwa na umati mkubwa wa wafuasi wake katika uwanja wa ndege wa Moi hapa Mombasa.

Alifanya ziara ya matembezi katika mitaa ya Changamwe, Jomvu, na Free Town iliyoko Kisauni.

Comments

comments