IEBC kuwahamisha makarani wa uchaguzi

0
1251

Mombasa,KENYA:Tume ya uchaguzi na mipakana nchini IEBC imesema itachapisha majina ya maafisa wake wakuu watakaohusika kuhesabu kura katika kaunti

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema majina hayo yatachapishwa wakati wowote.

Aidha maafisa wa uchaguzi pia watapewa uhamisho ili kuzuia mazoeya na wapiga kura.

Akiongea huko Limuru alikohudhuria kongamano la uwiano, Chebukati anasema anaelewa kibarua kigumu ambacho anacho kuhusu uchaguzi mkuu ujao.

Lakini amewataka wakenya kutokuwa na hofu akisema tume hiyo ina uwezo wa kusimamia kikamilifu uchaguzi huo.

Comments

comments