Uhaba wa maji wakumba mji wa Hola-Tana River

0
1799

Tanariver,KENYA:Mashirika ya kijamii kaunti ya Tana River yanalalamikia huduma duni za maji katika mji wa Hola.

Kulingana na mwenyekiti wa shirika la kijamii la TRiCCA eneo hilo Frankheart Daido wananchi eneo hilo wanahangaika kutafuta maji.

Kufikia sasa kulingana na mwenyekiti huyo wananchi wanatumia maji ya mto Tana moja kwa moja.

Tatizo hilo limedaiwa kuzidi siku chache baada ya kituo cha kusambaza maji cha Hola kukatiwa nguvu za umeme kufuatia limbikizi la deni.

Hata hivyo mkurugenzi wa kaunti wa idara ya maji Madubi Gwiyo, alisema serikali inaweka mikakati ya kulipa deni hilo la umeme ili kuendelea na huduma za kawaida kufikia leo.

Comments

comments