Washukiwa wa ulanguzi wa pesa wakamatwa Mombasa

0
1245

Mombasa, KENYA:Idara ya usalama mjini Mombasa inasema imewakamata washukiwa wawili wa uhalifu wanaohusishwa na ulanguzi wa pesa.

Kulingana na kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki, maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ulanguzi wa pesa, waliwanasa washukiwa hao baada ya kufuatilia mawasiliano yao ya simu.

Achoki alisema mmoja wa wahalifu aliwasili mjini Mombasa kutoka jijini Nairobi kwa lengo la kununua gari ambapo mwenye gari alitoa taarifa kwa maafisa wa polisi.

Achoka aliongeza kuwa washukiwa hao walifanikiwa kuwalagahi wakenya takribani shilingi milioni 2.8 chini ya muda wa miezi mitatu iliyopita kupitia malipo ya huduma ya simu ya M-pesa.

Imeharirirwa na Joseph Jira

Comments

comments